Utangulizi
Mfumo huu unamuwezesha mwananchi kutumia teknolojia mbalimbali kulingana na uwezo na mazingira yake, Mfumo umejumuisha matumizi ya SMS, Mobile Apps na Web.

Hali ilivyokuwa kabla ya kuundwa kwa mfumo huu
Mwananchi alitakiwa kwenda yeye mwenyewe kwenye Ofisi husika Mfano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri, Ofisi za Maafisa Tarafa, Ofisi za Kata na Ofisi ya Serikali ya Mtaa, ambapo mwananchi alilazimika kutumia gharama za nauli pamoja muda wake kufika Ofisini kuwasilisha malalamiko yake na kufuatilia. Kwa ujumla mchakato ulikuwa ni ‘manual system’,

Hali ilivyo baada ya kuanza kutumika kwa Mfumo
Mfumo huu umerekebisha mchakato mzima wa kushughulikia malalamiko ya wananchi, ambapo kwa sasa malalamiko yanawasilishwa kiteknologia ‘automation and digitization of the entire process’. Mwananchi anawasilisha malalamiko yake kwa njia ya SMS, Web na Mobile App au ikiwa amefika Ofisini yeye mwenyewe ambapo taarifa zake zitaingia kwenye Mfumo na kwenda moja kwa moja kwenye Idara husika.

Faida za Mfumo kwa Wananchi, Viongozi na Watumishi

Kwa Wananchi
Kwa kutumia Mfumo huu wananchi hawalazimika kufika Ofisini (labda pale itakapo lazimika kufanya hivyo) ili waweze kuwasilisha malalamiko yao, badala yake Mfumo utawawezesha wananchi kuwasilisha malalamiko yao; pia utawawezesha kufuatilia ili kujua hatua iliyofikiwa katika kushughulikia malalamiko yao kwa njia ya SMS, Web na Mobile App.

Kwa Viongozi na Watumishi
Mfumo huu unawezesha Viongozi na watumishi kuyafanyia kazi malalamiko yaliyowasilishwa kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kuwezesha kufanya ufuatiliaji na kujua kila hatua iliyofikiwa tangu malalamiko yalipo sajiliwa mpaka ufumbuzi ulipopatikana.
Aidha, mfumo huu unawezesha viongozi kuona hatua mbalimbali za malalamiko kadri yanavyo fanyiwa kazi na kutoa ushauri ipasavyo ikiwa ni pamoja na kupata taarifa kwa nyakati tofauti tofauti kadri zitakavyo hitajika. Kwa ujumla umeongeza uwazi na uwajibikaji kwa watendaji katika ngazi zote.
© 2019 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa